Timu ya taifa ya Congo imeibuka kidedea baada ya kuichapa timu ya taifa ya Burkina Faso kwa magoli mawili kwa moja katika mtanange wa michuano ya kombe la mataifa barani afrika inayoendelea kutimua vumbi huko nchini Equatorial Guinea.
ilikuwa ni Congo iliyoanza kupata bao katika dakika ya 52 ya mchezo kwa kupitia mchezaji Thievy Bifouma ambalo lilidumu mpaka dakika ya 86 ambapo mchezaji Aristide Bance aliweza kuisawazishia Burkina faso, lakini dakika ya 87 mchezaji Fabrice N'Guessi Ondama alipeleka kilio kwa mashabiki wa Burkina Faso baada ya kukwamisha mpira wavuzi na kuipa Congo goli la ushindi.
katika mchezo mwingine wenyeji timu ya taifa ya Equatorial Guinea imeendelea kuitumia ardhi ya nyumbani vyema baada ya kuibugiza timu ya taifa ya Gabon magoli mawili kwa ubuyu shukrani za pekee zikiwaendea Javier Balboa aliyefunga goli katika dakika ya 55 ya mchezo kwa mkwaju wa penalti na Iban Salvador Edu akipigilia msumari wa mwisho kunako dakika ya 86 ya mchezo.
0 comments:
Post a Comment