Thursday, January 1, 2015


NA MWANDISHI WETU, TANGA.
TIMU ya Coastal Union imeanza maandalizi kabambe ya kuhakikisha inajipanga vema ili kuhakikisha timu hiyo inapata pointi tatu muhimu kwenye mechi yake ya Ligi kuu dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Jumamosi wiki hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kutokana na umahiri wa kikosi
cha timu hiyo.

Akizungumza  leo mara baada ya kumalizika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly, Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wao dhidi ya Tanzania Prison tayari Kocha wao mkuu Mkenya  James Nandwa alikwisha kuyafanyia kazi na sasa kikosi kipo kamili kuwavaa maafande hao.

Amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni mzuri kwa sababu tayari,Kocha Mkuu wa timu hiyo,Mkenya James Nandwa alikwisha fanyia kazi kubwa ya kukiandaa timu hiyo na ataingia kwenye mechi hiyo akiwa na lengo moja
la kuhakikisha ushindi unapatikana ili kuweza kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara.

Hata hivyo amesema hakuna mchezaji hata mmoja ambaye ni majeruhi na kuwataka wapenzi na mashabiki kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kwenye mechi hiyo itakayochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video