Na Mwandishi Wetu, Tanga
TIMU ya Coastal Union imeondoka mkoani Tanga leo imeondoka alfajiri kuelekea Mkoani Shinyanga ikiwa na wachezaji 20, walimu wawili na viongozi wa timu hiyo tayari kwa kucheza mechi yao ya Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Stand United itakayopigwa kwenye uwanja wa Kambarage mjini humo.
Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa wiki endi hii ikiwa ni muendelezo wa michuano ya Ligi kuu soka Tanzania Bara ambapo timu hiyo itaingia uwanjani hapo ikiwa na matumaini ya kuweza kufanya vema baada ya kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza
Msafara wa timu hiyo unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union, Albert Peter ambaye amesema kuwa mara baada ya kuwasilia mkoani humo watafanya mazoezi madogo madogo kabla ya mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa Jumamosi wiki hii.
Akizungumzia hali za wachezaji wa timu hiyo, Kocha Mkuu, Mkenya James Nandwa amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mechi hiyo ili kuweza kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi kuu.
Amesema kuwa licha ya michuano hiyo kuwa na upinzani mkubwa lakini wao wamejithatiti vilivyo ili kuweza kucheza kwa umakini ambao utawawezesha kupata matokeo mazuri.
Hata hivyo amewataka wapenzi na mashabiki wa soka mkoani Tanga wanaoishi mkoani Shinyanga kujitokeza kwa wingi kwenye mechi hiyo lengo likiwa kuwapa hasama wachezaji wa timu hiyo.
Timu ya Coastal Union itaingia kwenye mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kupata sare kutokufungana nyumbani dhidi ya Polisi Morogoro ambapo hivi sasa ina pointi 13 ikiwa nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi
kuu.
0 comments:
Post a Comment