
ALIYEKUWA nahodha wa Simba, Mganda, Joseph Owino amerejea
kwao Uganda kwa madai ya kutofautiana na kiongozi mmoja wa juu wa Simba.
Taarifa kutoka chanzo makini zinaeleza kuwa Owino
aliingia kwenye mgogoro na viongozi wa Simba Oktoba 25 mwaka jana baada ya
kumuamuru kipa kinda Peter Manyika alale chini dakika za majeruhi katika mechi
ya ligi kuu Tanzania bara waliyotoka sare ya 1-1- na Tanzania Prisons uwanja wa
Sokoine.
Manyika kwa kufuata maelekezo ya nahodha wake
Owino, alilala chini, lakini akajishitukia
na kutaka kusimama na ndipo akakutana na mpira wa juu ambao alishindwa kupangua
na kufungwa goli rahisi.
Manyika alipoulizwa kwanini alilala, alimjibu
kocha Patrick Ackson Phiri na viongozi wa Simba akisema aliaambiwa na Owino alale
chini.
Viongozi wa Simba walikasirika ikikumbukwa
walikuwa na ugonjwa wa ‘sare sare maua’ na walitaka kuvunja mkataba wa Owino,
lakini kocha Phiri alimtetea sana na kusema bado anamhitaji.
Phiri aliwahi kukiri kuwepo kwa mvutano wa Owino
na viongozi, lakini alisema kutokana na kumtetea beki huyo wa kati wakakubali
kwa shingo upande na kuagiza asajiliwe beki mwingine na ndipo akaletwa Juuko
Mursheed.
Viongozi wa Simba hawakutaka Owino acheze, badala
yake walihitaji Mursheed na Isihaka wasimame katika ngome ya ulinzi.
Baada ya kuondoka kwa Phiri kumemaliza kila kitu
na kuna uwezekano mkubwa Owino asicheze tena Msimbazi.
0 comments:
Post a Comment