Timu ya taifa ya Zambia almaarufu kama Chipolopolo imetupwa nje ya michuano ya kombe la mataifa barani Afrika baada ya kulazimishwa sare ya kutokufungana dhidi ya timu ya taifa ya Cape Verde ambayo pia imelazimika kuyaaga mashindano hayo baada ya sare hiyo.
Zambia ilikuwa na matumaini ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo lakini hali iliwaendea ndivyo sivyo na kujikuta ikipoteza nafasi nyingi za wazi na kushindwa kukwamisha mpira wavuni.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo timu ya taifa ya Tunisia imeweza kutoshana nguvu na DR Congo baada ya kufungana goli moja kwa moja na kufanikiwa kufuzu katika hatua inayofuata ya michuano hiyo inayoendelea kutimua nchini Equatorial Guinea.
0 comments:
Post a Comment