Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Wakati Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) iko ukiongoni, timu za Burkina Faso na Oljoro JKT zimefanya 'mauaji' baada ya kutoa vipigo vikubwa katika mechi za jana za michuano hiyo.
Burkina Faso ya Morogoro iliyo Kundi B linaloongozwa na Mwadia FC ya Shinyanga, iliichapa Rhino Rangers ya Tabora mabao 4-0 mjini Morogoro wakati Oljoro JKT ya Arusha iliyo Kundi B pia ikichapa Toto Africans ya Mwanza mabao 3-0 mjini Arusha jana.
Katika Kundi A, wapinzani wakuu wa Coastal Union jijini Tanga, timu ya African Sports ilitungua JKT Mlale ya Ruvuma bao 1-0 mjini Tanga wakati Police Tabora ikinga'ra kwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Kanembwa ya Kigoma mjini Tabora katika mechi nyingine ya Kundi B jana .
Geita Gold FC ya mkoani Geita iling'ang'aniwa baada ya kulazimishwa suluhu dhidi ya Panone FC ya Kilimanjaro (Kundi B) wakati Police Mara ikishikwa pia kwa suluhu dhidi ya maafande wenzao wa Polisi Dodoma (Kundi B) pia.
Kwa matokeo hayo Mwadui FC ya Shinyanga ambayo juzi ilishinda 2-1 dhidi ya Green Warriors ya Dar es Salaam, inaongoza Kundi ikiwa na pointi 40, moja mbele ya Toto Africans iliyoko nafasi ya pili ikifuatwa na Oljoro JKT (35) sawa na Polisi Tabora inavyoonekana katika msimamo hapo chini.
Na. Timu Pld W T L GF GD Pts
1 A/Sports 20 14 2 4 25:14 11 43
2 Majimaji 19 10 6 3 23:13 10 36
3 Friends 19 9 8 2 22:13 9 35
4 Lipuli 19 9 8 2 16:8 8 35
5 Kimondo 19 8 3 8 19:20 -1 27
6 Ashanti 19 6 5 8 23:27 -4 23
7 Kurugenzi 18 5 7 6 17:18 -1 22
8 Tessema 18 6 4 8 10:14 -4 22
9 JKT Mlale 19 4 7 8 16:18 -2 19
10 Polisi Dar 18 3 6 9 14:20 -6 15
11 A/Lyon 19 3 5 11 14:21 -7 14
12 V/Squad 19 3 5 11 10:23 -13 14
MSIMAMO KUNDI B FDL
Na. Timu Pld W T L GF GD Pts
1 Mwadui 20 11 7 2 34 20 40
2 Toto 20 12 3 5 31 14 39
3 Oljoro 19 10 5 4 30 12 35
4 Polisi Tbr 19 10 5 4 17 8 35
5 Geita 19 7 4 8 19 1 25
6 Panone 19 5 9 5 13 -1 24
7 Kanembwa 19 6 5 8 11 -10 23
8 Rhino 19 5 7 7 11 -7 22
9 Bukinafaso 20 3 10 7 18 2 19
10Polisi Mara 18 4 8 6 18 -8 19
11 Polisi Dom 20 3 7 10 9 -15 16
12 G/Warriors18 2 4 2 16 -15 10
Shukrani kwa Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa matokeo taarifa zote zinazohusu FDL anazoupatia mtandao huu.
0 comments:
Post a Comment