Daley Blind aliifungia goli timu yake dhidi ya West Bromwich Albion
VIDEO za Daley Blind zimewekwa You Tube zikionesha magoli ya ajabu aliyofunga, ujuzi, pasi na 'Tackles' anazopiga.
Ukweli ni kwamba video hizo zimejumuisha na goli moja aliloifungia Manchester United United dhidi ya West Brom mwezi Oktoba mwaka jana.
Blind akipozi katika picha na jezi yake baada ya kujiunga na Manchester United, akiungana na Louis van Gaal na Radamel Falcao.
Blind jana amekutana na waandishi wa Uingereza na aliulizwa kuhusu maoni ya Gary Neville ambaye alisema hachezi vizuri, anacheza sana pasi mraba ambazo hazina madhara kwa wapinzani.
Akizungumzia maneno hayo ya nahodha huyo wa zamani wa Manchester United, Blind amekiri kuyasikia vizuri.
"Kiukweli, nilimsikiliza lakini najaribu kucheza mchezo wangu na vile anavyotaka mwalimu ambapo anataka kumiliki mpira".
"Siku zote kuna wanaotaka kuwazungumzia walimu au timu, vinginevyo TV zao hazitakuwa na mvuto".
"Naweza kuchukua kidogo ukosoaji. Watu wa TV wanasema wanachotaka. Unasikiliza, lakini nadhani nimecheza vizuri kwenye baadhi ya mechi"
0 comments:
Post a Comment