Friday, January 9, 2015



Na Bertha Lumala
ANAFAHAMIKA sana visiwani Zanzibar kwa jina la JANJA. Huyu si mwingine, bali ni Amour Omary, mfungaji wa bao pekee la mechi kali kati ya Yanga SC na JKU FC Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Unajua alichokisema baada ya kuing'oa timu hiyo ya Jangwani katika michuano hiyo ya tisa ya Kombe la Mapinduzi" Tega sikio!

Ikiwa inapumlia mashine kutokana na uimara wa kikosi cha Yanga SC kilichokuwa kikicheza nusu uwanja, JKU FC ilifanya shambulizi la kushtukiza langoni mwa wanajangwani dakika ya 72, beki wa pembeni Oscar Joshua alipozubaa na kumpa nafasi kiduchu ya kupiga shuti mshambuliaji huyo.

Pengine kutokana na kutomjua vizuri, lakini Yanga SC ilipaswa kujua kwamba Janja ni kinara wa mabao katika Ligi Kuu ya Zanzibar msimu huu akiwa ametupia mara nane huku pia akiwa na taji la mfungaji bora wa ligi hiyo msimu uliopita.

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm na msaidizi wake Boniface Mkwasa hawajakosa hata mechi moja kwenye Uwanja wa Amaan, kila mechi walioneakana Jukwaa la VIP wakisoma mbinu za wapinzani. Hakika walipaswa kumjua mkali huyu wa mabao!

Kabla ya mechi hiyo, Janja alikuwa amefunga mabao magumu na maridhawa, moja dhidi ya Mafunzo waliposhinda 2-0 katika mechi yao ya Kundi C na jingine katika mechi yao ngumu ya mwisho ya Kundi C dhidi ya Mtibwa Sugar iliyomalizika kwa sare ya 1-1.

Kosa la Joshua kuukimbia mpira akitaka aubutue kwa mguu badala ya kuupiga kichwa, likaigharimu Yanga SC mbele ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi aliyekuwa mgeni rasmi.

Yanga SC iliyokuwa inapewa nafasi kubwa ya kutinga fainali ya michuano hiyo na kuchuana na timu inayoonekana kama kuunga unga katika michuano hiyo ya Simba SC, sasa inatakiwa kurejea Dar es Salaam kabla ya Januari 14 kama ilivyotarajiwa hapo awali. 

Hakuna jinsi inabidi tu warejee kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kujiandaa kwa mechi zao za kiporo dhidi ya Mbeya City na Coastal Union kabla ya kutimkia Zambia kushiriki mashindano maalum ya kimataifa na kuipashia misuli michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika itakayoanza mwezi ujao wakichuana na BDF XI.

Mara tu baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa, Janja alimkimbilia kocha wake, Malale Hamsin Keya na kumkumbatia huku akilia kwa furaha. Naam, kweli yalikuwa machozi ya furaha ukizingatia bao lilikuwa gumu na amelifunga kwa mguu wake anaoumini wa kushoto.

"Nimekuwa mchezaji kwa muda mrefu sasa, kazi yangu ni kufunga. Yanga walitubana sana lakini kama mshambuliaji nilituliza akili vilivyo kabla ya kupiga shuti lile. 

"Ilikuwa nafasi nzuri kwetu baada ya Yanga kujisahau kidogo kutokana na kutushambulia muda wote. 

"Mazoezi na kuzingatia maeklezo ya mwalimu wangu (Malale) ndiyo siri ya mafanikio yangu," amesema Janja.

........................itaendelea 
ENDELEA KUFUATILIA MTANDAO HUU

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video