Wednesday, January 28, 2015






Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale amesema hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo na kujiunga na Manchester United kwani bado anafuraha kuwa katika dimba la Santiago Bernabeu licha ya kuhusishwa na kujiunga na mashetani wekundu dimbani old Trafford.
 
 lakini winga huyo mwenye miaka 25 ameweka wazi sasa kuwa hafikiri kurudi kucheza ligi kuu nchini Uingereza hasa katika klabu ya Manchester United, na sasa nguvu zake zote anazilekeza katika ligi kuu nchini Uhispania almaarufu na La Liga na kushindania namba katika kikosi cha kwanza cha Carlo Ancelloti.

"Sidhani kama naweza kurudi kucheza ligi kuu nchini Uingereza eti kujiunga na Manchester United hapana, nina furaha kuichezea Real Madrid na ninafanya juhudi kuhakikisha nalinda namba yangu katika kikosi cha kwanza siku zote," alisema Bale alipoulizwa swali na gazeti la Cadena.
mpaka sasa Bale ameshafunga magoli 12 katika mechi 26 alizocheza msimu huu

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video