Friday, January 23, 2015

Shakes Mashaba
KOCHA wa Bafana Bafana, Ephraim Shakes Mashaba amesema kikosi chake kinafahamu kuwa hakuna matokeo mengine yanayohitajika dhidi ya Senegal zaidi ya ushindi tu.
Afrika kusini leo usiku  inachuana na Senegal katika mechi ya pili ya kundi C ya kombe la mataifa ya Afrika kwenye uwanja wa Stade de Mongomo nchini Guinea ya Ikweta. 
Bafana Bafana wanaingia katika mechi hiyo wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha 3-1 walichopata dhidi ya Algeria katika mechi ya kwanza na wanahitaji ushindi tu. Senegal waliifunga Ghana 2-1 kwenye mechi ya ufunguzi.
"Hakuna namna ya kujifanya hatuna presha kwasababu ushindi tu ndio unahitajika. Lakini kila mmoja yupo kwenye presha, hata wapinzani wetu. Tupo katika hali sawa licha ya wao kuwa na faida ya pointi tatu walizovuna mechi ya kwanza na hawatachukulia mechi hii kirahisi. Watakuwa wanatema cheche kama sisi kwasababu tunahitaji kushinda ili tuwe mazingira mazuri ya kutelekeza mipango yetu katika mashindano haya," Amesema Mashaba.
"Mechi itakuwa ngumu sana. Wote tunahitaji pointi kwasababu kama tutawafunga tutakuwa pointi sawa. Vijana wetu wapo tayari, tumewaambia kinachohitajika na wamesema watu wasiangalie zaidi matokeo yaliyopita"
Kikosi SA 11 vs Algeria: 22-Jackson Mabokgwane (GK), 6-Anele Ngcongca, 11-Thabo Matlaba, 14-Thulani Hlatshwayo, 3-Eric Mathoho, 15-Dean Furman (C), 5-Andile Jali, 20-Oupa Manyisa, 18-Thuso Phala, 10-Sibusiso Vilakazi, 23-Tokelo Rantie
Wachezaji wa akiba: 16-Darren Keet (GK), 1-Brilliant Khuzwayo (GK), 21-Ayanda Gcaba, 13-Thamsanqa Sangweni, 19-Themba Zwane, 12-Reneilwe Letsholonyane, 7-Mandla Masango, 8-Bongani Zungu, 17-Bernard Parker, 4-Siyabonga Nhlapho, 9-Bongani Ndulula
Majeruhi: 2-Rivaldo Coetzee.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video