KUFUATIA kuifunga Simba Sc mabao 2-1 katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyopigwa jana uwanja wa Taifa, kocha mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi ametoka kauli ya kumshukuru Mungu kwa kuiwezesha City kupata pointi tatu muhimu ambazo zitaifanya kusogea katika nafasi nyingine kwenye msimamo wa ligi huku. Pia amewashukuru wachezaji na mashabiki waliosafiri kutoka Mbeya kuja kuisapoti timu yao.
“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kupata ushindi, hizi ni pointi tatu muhimu ambazo zitatusogeza kwenye nafasi nyingine katika msimamo wa ligi, nawashukuru mashabiki wetu waliosafiri kutoka Mbeya kuja hapa kutupa sapoti, nafahamu mwishoni mwa juma hili tuna mchezo mwingine wa ligi dhidi ya Polisi Morogoro tunaanza maandalizi ya mchezo huo leo kuhakikisha tunapata matokeoa na kwa uwezo wa Mungu naamini tutafanikiwa” amesema Mwambusi
0 comments:
Post a Comment