Sunday, January 4, 2015

Kikosi cha Azam kilichoanza leo

AZAM FC imewalaza bao 1-0 mabingwa watetezi wa Zanzibar, KMKM, katika mchezo wa kombe la Mapinduzi uliomalizika usiku huu uwanja wa Amaan Zanzibar.

Huo ni ushindi wa kwanza kwa Azam fc baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa awali dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi KCCA ya Uganda.

Bao pekee la Azam lilipatikana katika dakika ya 18 kutokana na nahodha wa KMKM, Khamis Ali kujifunga kwa kichwa akijaribu kuokoa mpira wa krosi uliochongwa na Shomari Kapombe.

Kikosi cha KMKM

Kiujumla timu zote zilicheza vizuri na kushambuliana kwa zamu, lakini Azam wameonekana kukosa mipango na kuzua hofu kwa mashabiki wao ikizingatiwa wanaenda kuwakilisha nchi katika michuano ya ligi ya mabingwa  Afrika sanjari na kutetea ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara..
Kocha mkuu wa Wanalambalamba hao, Mcameroon, Joseph Marius Omog amekiri ugumu wa KMKM .

"Tulikutana nao Kigali kombe la Kagame, ni wapinzani wa kweli. Wameimarika, lakini timu yangu imejitahidi kucheza vizuri". Alisema Omog.

Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za mwisho za kundi C ambapo Mafunzo watakabiliana na Mtibwa Sugar majira ya saa 10:00 jioni uwanja wa Amaan.


Majira ya saa 2:15 usiku katika uwanja huo huo, Simba watashuka dimbani kuchuana na JKU.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video