Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Azam FC jana kilichapwa bao 1-0 na TP Mazembe katika mashindano maalum ya kimataifa yanayoendelea nchi DR Congo.
Habari kutoka DRC ambazo mtandao huu umezipata zinaeleza kuwa katika mashindano hayo yanayoshirikisha timu nne; wenyeji TP Mazembe, Zesco ya Zambia, Don Bosco na Azam FC, wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa wameanza kwa kichapo hicho.
Mechi ya TP Mazembe dhidi ya Azam FC ilianza saa 11 jioni jana ikitanguliwa na mechi ya Don Bosco dhidi ya Zesco.
Endelea kufuatilia mtandao huu, tutakujuza zaidi matokeo ya mechi zote za jana, wafuyngaji na yote yanayojiri DRC.
Michuano hiyo itamalizika Febrauri 3 na Azam FC wanaitumia kujiandaa kwa mechi zao za Klabu Bingwa dhidi ya mabingwa mara 19 wa Ligi Kuu ya Sudan, klabu ya El-Merrikh.
0 comments:
Post a Comment