Tuesday, January 6, 2015

SAM_4229
Kocha mpya wa Simba sc

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Awadh Issa Juma amekiri wazi kuwa kocha mpya wa timu hiyo, Mserbia, Goran Kopunovic ameleta mbinu mpya katika timu yao.

Awadh aliyasema hayo baada ya Simba kufuzu robo fainali ya kombe la Mapinduzi kufuatia kuitandika JKU bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Amaan usiku wa jana.

Bao hilo pekee lilifungwa kwa shuti kali na Ramadhan Singano ‘Messi’ katika dakika ya 11 ya kipindi cha kwanza akimalizia pasi nzuri ya Said Ndemla.

Katika mechi ya kwanza, Simba walifungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar, mechi ya pili wakashinda 1-0 dhidi ya Mafunzo na ushindi wa jana umewafanya wajikusanyie pointi 6 na kuibuka vinara wa kundi C.

Awadh alisema kwasasa wanafanya mazoezi magumu kwa lengo la kutafuta nguvu na kasi, hivyo watarudi vizuri ligi kuu.

“Kila kitu kimebadilika. Mwalimu amekuja na mbinu mpya. Kwasasa tupo katika mazoezi magumu, ndio maana tulianza kwa kasi kipindi cha kwanza, lakini kipindi cha pili kasi ilipungua”. Alisema Awadh.

“Tumempa muda mwalimu na tunaamini atatufikisha mbali katika michuano ya ligi kuu”.


Simba kwa sasa inafanya mazoezi mara mbili, inaanzia uwanjani na inamalizia ufukweni.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video