Wednesday, January 7, 2015


Kiungo wa Cameroon na West Ham Alex Song amestaafu kucheza soka la kimataifa baada ya kutotajwa katika kikosi cha timu ya taifa kitakachocheza Kombe la Mataifa ya Afrika. Kiungo huyo, 27, anayecheza kwa mkopo kutoka Barcelona sasa ataweza kuendelea kuichezea West Ham baada ya mazungumzo ya dakika za mwisho na Cameroon kuvunjika. Kupitia Instagram amesema: "Mapenzi yangu kwa nchi yangu hayatobadilika. Nataka kuchukua muda na kuelekeza nguvu zangu kujenga tena fani yangu West Ham United". Song hajaichezea timu yake ya taifa tangu alipopewa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya Croatia katika ngazi ya makundi katika Kombe la Dunia 2014. West Ham walikuwa na wasiwasi wa kumkosa mchezaji huyo baada ya kwenda Cameroon kujadili uwezekano wa kujumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa, kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoanza Januari 17 nchini Equatorial Guinea.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video