Klabu ya Fiorentina inayoshiriki ligi kuu nchini Italia kwa
kupitia mtandao wa klabu hiyo imedhibitisha rasmi kumsajili kwa mkopo mchezaji
wao wa zamani Alberto Gilardino kutoka katika klabu ya Guangzhou Evergrande
ambapo ataitumikia klabu hiyo mpaka mwisho wa msimu huu, lengo kubwa ikiwa ni
kusajiliwa na klabu hiyo moja moja mwisho wa msimu.
Gilardino ameshawahi kuichezea Fiorentina mwaka 2008 hadi
mwaka 2012, na kuifungia magoli 59 katika mechi 143 alizocheza.
0 comments:
Post a Comment