Wednesday, January 7, 2015


Mwandishi Wetu, Zanzibar
TIMU ya Kikapu ya African Magic imepewa ushindi bila ya jasho baada ya juzi wapinzani wake JKU kutofika uwanjani katika mashindano inashiriki michuano ya kikapu ya Kombe la Karume visiwani hapa.

Kutokana na kutoonekana kwa kikosi cha JKU kwenye Uwanja wa Maisara juzi, kamati ya mashindano hayo iliamua kuipa African Magic ushindi wa vikapu 20 na pointi mbili.
Baadaye saa 11:00 jioni kwenye uwanja huo kulichezwa mechi ya kikapu ya Polisi dhidi ya Stone Town ambayo maafande wa Polisi walishinda vikapu 46-42. 

Katika hatua nyingine, timu ya netiboli ya Mafunzo imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Mapinduzi la mchezo huo kwa ushindi wa 45-39 dhidi ya KVZ kwenye Uwanja wa Gymkanah visiwani hapa.

Mafunzo ilionekana imepania kushinda baada ya kuongoza katika robo ya kwanza ya mchezo huo maalum kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanywa Januari 12, 1964.

Katika mchezo huo mafunzo ilimaza robo ya kwanza ikiongoza 13-6, robo ya pili 26-13 huku robo ya tatu ikimaliza magoli 34-22. 

Bingwa wa mchezo huo ulioandaliwa na Chama cha Netiboli Zanzibar (Chaneza) ambao mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Thuwaiba Edington, alizawadiwa Sh. 150,000 na wa pili Sh. 100,000.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video