Friday, January 23, 2015

MECHI za raundi ya pili ya Kundi C ambalo linaaminika kuwa la kifo katika michuano ya mataifa ya Afrika, Afcon 2015 inayoendelea nchini Guinea ya Ikweta zitapigwa leo majira ya saa 1:00 na saa 4:00 usiku.
Mechi ya kwanza itawakutanisha Ghana dhidi ya Algeria.
Mtanange huu umevuta hisia za mashabiki wengi Afrika kutokana na ubora wa vikosi vyao.
Ghana walipoteza mechi ya kwanza kwa kufungwa mabao 2-1 na Simba Wateranga Senegal, wakati Algeria walishinda 3-1 dhidi ya Afrika kusini na mpaka sasa ndio timu pekee iliyofunga mabao mengi katika mechi moja.
Mechi ya pili itaanza saa 4:00 usiku baina ya timu ya taifa ya Afrika kusini 'Bafana Bafana' dhidi ya Senegal.
Jana usiku zimeshuhudiwa mechi mbili za kundi B ambapo mechi moja ya kwanza,  Zambia walichuana na Tunisia.
Miamba hiyo ya kaskazini mwa Afrika iliwatandika Chipolopolo mabao 2-1.
Baada Cape Verde walitoka suluhu na DRC Congo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video