Hatimaye Anderson anaweza kuondoka Old Trafford
KIUNGO wa Manchester United asiyekuwa fiti, Anderson anaingia kwenye mazungumzo ya kumaliza maisha yake ya soka Old Trafford na kurudi kwao Brazil.
Klabu ya Internacional ya Brazil imeshawasiliana na United pamoja na wawakilishi wa mchezaji ambapo mazungumzo zaidi yamepangwa kuanza leo ijumaa asubuhi.
Anderson hana nafasi katika kikosi cha Louis Van Gaal na hata wakati wa David Moyes alitolewa kwa mkopo katika klabu ya Fiorentina.
Anderson, hajawahi kucheza tena tangu alipoingia dakika 20 za mwisho dhidi ya Burnley mwezi wa nane mwaka jana na sasa anauzwa.
Nyota huyo mwenye miaka 26 hajaonesha thamani yake tangu alipotua Old Trafford kutokea Porto sambana na Nani kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 26 mwaka 2007.
Anderson anaelekea kumaliza mkataba wake na United wanafikiria kuuvunja, lakini Internacional wanaweza kukubali kumnunua.
0 comments:
Post a Comment