Monday, December 29, 2014

Screen Shot 2014-12-28 at 10.50.38 PM

KIKOSI cha Yanga leo jioni kimeshindwa kukamilisha ratiba yake ya kufanya mazoezi kutokana na mvua kubwa na sasa kitaondoka kesho asubuhi kuelekea kambini Mkoani Bagamoyo.

Akizungumza na mtandao huu kocha wa Yanga Hans Pluijm amesema kikosi chake kilikuwa  na ratiba ya kufanya mazoezi mepesi katika Uwanja wao wa Kaunda uliopo makao makuu ya klabu yao lakini mvua kubwa iliyonyesha leo asubuhi jijini Dar es Salaam imeujaza maji uwanja huo.

Pluijm  amesema baada ya mabadiliko hayo sasa kikosi hicho kitaingia kambini rasmi kesho asubuhi katika hoteli ya Kiromo ambapo ratiba ya mazoezi yao itaendelea siku hiyo jioni.

"Tumeshindwa kufanya mazoezi leo mvua imejaza maji pale uwanja wa klabu, nilitaka wachezaji wafanye mazoezi mepesi baada ya mchezo wa jana lakini sasa limeshindikana,"alisema Pluijm.


"Tunaondoka kesho asubuhi kwenda kambini Bagamoyo kuanza maandalizi ya mechi zijazo tutaraji ratiba ya mazoezi yetu itaendelea hiyo kesho.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video