Monday, December 29, 2014

YANGA imethibitisha kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi inayotarajia kuanza kutimua vumbi januari Mosi mwakani.

Makamu mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amesema mwaka jana hawakupeleka timu Zanzibar, kitendo ambacho kilitafsiriwa vibaya na Wazanzibar mpaka walipoenda kuomba msamaha.

Sanga amesema hawataki tena kurudia makosa, hivyo watapeleka kikosi cha kwanza katika michuano hiyo.

Wakati huo huo nao Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, Azam fc wamethibitisha kupeleka kikosi cha kwanza katika michuano ya Mapinduzi.

Afisa mtendaji mkuu wa  Azam fc, Sady Kawemba amesema michuano hiyo ni fursa kwao kuendelea kujiandaa na michuano ya ligi na ligi ya mabingwa Afrika.


Taarifa zinaeleza kuwa wapinzani wa Azam katika ligi ya mabingwa Afrika, Al Merreick ya Sudan nao wanaomba kushiriki michuano hiyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video