Tuesday, December 30, 2014

Kusajiliwa kwa mlinda mlango wa zamani wa Kagera Sugar Hanington Kalyesubula kumeibua vita kubwa ya kuwania  namba  katika kikosi cha Mbeya City Fc miongoni mwa magolikipa watatu waliopo sasa.
Akizungumza  mapema leo  mlinda mlango David Buruhani  aliyeshikiria namba moja katika kikosi hicho kwa muda mrefu amesema kuwa amelazimika kuongeza juhudi zaidi ili kumshawishi mwalimu Juma Mwambusi kuendelea kumtumia kama chaguo la kwanza kufuatia ujio wa Hanington na pia umahiri unaonyeshwa mazoezini hivi sasa na kipa namba mbili wa City Lambony Ashery.
“Ujio wa Hanington umeleta changamoto mpya kwenye nafasi yetu, na Ashery hivi sasa anafanya vizuri mazoezini, nimelazimika kuongeza juhudi kwa kufanya mazoezi ya ziada ili kuendelea kumshawishi mwalimu  nibaki kuwa kipa chaguo la kwanza kwa sababu nina kiu ya kudhihirisha ubora wangu  kwenye michezo ya sasa kufuatia mwanzo mbaya kwenye  mechi saba za mwanzo.” alisema David.
Akiendelea zaidi kipa huyo anayeshikiria rekodi ya kucheza michezo mingi zaidi miongoni mwa nyota wanaounda kikosi cha City alisema kuwa  hivi sasa timu imekuwa na kikosi kikubwa na chenye ushindani wa hali ya juu katika kuwania nafasi ya kikosi cha kwanza kwa wachezaji wote  jambo ambalo linamfanya kuamini kuwa Mbeya City itafanikiwa kupata matokeo mazuri tena mwisho wa msimu huu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video