Tuesday, December 30, 2014


Umony
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam

Mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Brian Umony ataikosa michuano ya Kombe la Mapinduzi mwakani, imefahamika.

Taarifa zilizochapishwa na mtandao wa Kawowo Sports wa Uganda leo zimeeleza kuwa timu ya Kampala City Council Football Club (KCC FC) itakosa huduma ya nyota huyo katika michuano hiyo mwakani kutokana na sababu mbalimbali.

Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 13 tangu arejee KCC FC akitoka Azam FC ameachwa katika ziara hiyo ya Zanzibar kutokana na majeraha na kutojua hatma yake ndani ya kikosi hicho.

“Tuko katika mazungumzo na Brian (Umony) kuona kama kuna uwezekano wa kumzuia asiondoke," amesema kocha Abdallah Mubiru. “Hayuko fiti asilimia 100 na ameomba aachwe katika ziara yetu ya Zanzibar jambo ambalo ni sahihi," ameongeza.
Ikumbukwe kuwa Umony yuko mbioni kujiunga na moja kati ya  mabingwa wa Kenya Gor Mahia na AFC Leopards bila kuisahau klabu ya St. George ya Ethiopia ambazo zote zinaiwania saini ya mshambuliaji huyo wa kati.

Umony anaungana na mabeki Habib Kavuma (malaria) na Isaac Ntege (taya) ambao hawaendi Zanzibar kutetea taji la Kombe la Mapinduzi.

Katika hatua nyingine, kikosi chenye wachezaji 21 cha KCC FC kinatinga Zanzibar kwa ajili ya michuano hiyo pamoja na Joseph Ochaya na Simon Mbaziira ambao wanatarajiwa kusaini mikataba kuitumikia klabu hiyo katika usajili wa Januari.

“Kuhusu Simon (Mbaziira), kila kitu kimekamilika lakini tunasubiri majibu ya Asante Kotoko kuhusu Ochaya,” alieleza Mubiru.

KCC FC bado haijatambua rasmi wapinzani wake katika kundi la michuano hiyo itakayoanza Januari Mosi huku timu mbili za Kenya AFC Leopards na Tusker SC tayari zikiwa zimejitoa na kuifanya michuano hiyo ibaki na timu 10.

Timu nyingine ni pamoja na mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC, Mtibwa Sugar FC, Simba SC, Yanga SC, mabingwa wa Zanzibar KMKM, Police FC, JKU, Mtende Rangers na Shaba FC.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video