Wednesday, December 31, 2014


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam 
Timu ya Ulinzi Stars ya Kenya imechukua nafasi ya Tusker FC waliojitoa kushiriki Kombe la Mapinduzi mwakani.

Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Haji Salum amesema Dar es Salaam leo kuwa timu hiyo itashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya Tusker FC na AFC Leopards, zote za Ligi Kuu ya Kenya kujitoa.

Nafasi ya AFC Leopards inatarajiwa kuchukuliwa na mabingwa mara 19 wa Ligi Kuu ya Sudan, El Merrikh ambao wametuma maombi ya kushiriki mashindano hayo mwakani.

Ratiba ya michuano hiyo iliyopangwa kufanyika kuanzia Januari 1-13 mwakani, Salum amesema itatoka rasmi kesho baada ya kuthibitishwa ushiriki wa El Merrikh.

Jumla ya timu 12 zimealikwa kushiriki michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya tisa tangu ianzishwe kuenzi Mapinduzi Tukufu ya Zanzibar yaliyofanyika Januari 12, 1964.

Mbali na timu nne za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Azam FC, Mtibwa Sugar FC, Simba SC na Yanga SC, wamo pia mabingwa watetezi KCC FC ya Ligi Kuu ya Uganda, mabingwa wa Zanzibar KMKM, Mafunzo FC, JKU FC, Mtendeni FC, Police Zanzibar na Shaba FC ya Pemba.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video