Wednesday, December 3, 2014


Na Bertha Lumala, Dar es salaam
TIMU ya soka ya The Express ya Uganda inatarajia kuwasili nchini kesho kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na timu za Simba na Yanga.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mratibu wa mechi hizo, George Wakuganda amesema kuwa baada ya mashabiki wa soka nchini kukaa muda mrefu bila kushuhudia mechi, wameona ni vyema kuileta timu hiyo ili kucheza na vigogo hivyo vya soka nchini.
“Kwa sasa timu zinafanya usajili katika kipindi cha dirisha dogo, hivyo tumeona ni vyema Simba na Yanga wakawajaribu wachezaji wao kabla ya kukutana Desemba 13, mwaka huu katika mechi ya Nani Mtani Jembe 2,” amesema Wakuganda.
Amesema The Express wataanza kucheza na Simba Ijumaa na kisha Yanga Jumamosi mechi zote zitachezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
ex
Amesema ni fursa nzuri kwa makocha wa pande zote mbili kuangalia upungufu kwenye vikosi vyao kabla ya mechi yao ya Desemba 13.
Wakuganda amesema ameshafanya mazungumzo na pande zote mbili za uongozi wa Simba na Yanga na wote wamekubali kucheza mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa.
Kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo Simba ilikuwa ikifanya mazungumzo na mchezaji Dan Ssemkuruma ambaye anatarajiwa kuwasili nchini leo kwa ajili ya kumalizana na klabu hiyo kutoka mitaa ya Msimbazi.
Kwa wachezaji wa ndani Simba inaonyatia kwa sasa ni Nurdin Choma wa Prisons ya Mbeya anayecheza nafasi ya beki wa kati na beki wa kulia Salum Kimenya wa Prisons pia. Simba pia inataka kuwabomoa Mbeya City kwa kumsajili kiungo mshambuliaji Deus Kaseke.
Endapo Simba itamalizana na wachezaji hao, Ijumaa wanaweza kuonekana uwanjani. Yanga itatumia nafasi hiyo kumtambulisha kiungo wao mpya Mbrazil Emerson De Oliveira Neves Roque.
Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mechi ya kwanza ya Nani Mtani Jembe iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Desemba 21, mwaka jana, kipigo ambacho kilitimua benchi lote la ufundi la Yanga lililokuwa chini ya kocha mkuu, Mholanzi Ernie Brandts, msaidizi wake Felix Minziro (sasa Kocha wa JKT Ruvu) na kocha wa makipa Mkenya Razak Ssiwa.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video