Wednesday, December 3, 2014

Zacharia Hans Poppe

KAMATI ya usajili ya Simba imeshindwa kupata beki wa kati kama walivyoagizwa na kocha mkuu, Mzambia, Patrick Phiri.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba sc, Zacharia Hans Poppe ameuambia mtandao huu kuwa kocha Phiri aliagiza apatikane beki wa kati wa kiwango cha juu, lakini wameshindwa kupata beki wa aina hiyo katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Poppe aliongeza kuwa inabidi kocha aendelee na mabeki waliopo kwa sasa.

Kepteini huyo wa zamani wa JWTZ aliongeza kuwa kocha aliagiza apatikane mshambuliaji mkali na wamefanikiwa kumsainisha miaka miwili nyota wa Gor Mahia ya Kenya, Mganda Danny Sserunkuma.

Aidha aliongeza kuwa wapo katika mazungumzo ya mwisho na nyota wa Polisi Morogoro Danny Mrwanda na Hassan Kessy wa Mtibwa Sugar.


Muda wowote kutoka sasa makubaliano na wachezaji hao yatafikiwa na kuwasainisha mikataba. 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video