Monday, December 29, 2014

Na Sanula Athanas
26th December 2014
Kauli kwamba “makocha wanaajiriwa ili wafukuzwe” ikimaanisha makocha wamekuwa watu wa kwanza kuchukuliwa hatua na uongozi pindi timu inapokuwa na matokeo mabovu, imekuwa ikionekana kuwa na mashiko wakati makocha wa timu mbalimbali wanapotimuliwa.
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) leo inaingia raundi ya nane zikiwa zimechezwa mechi 49 yakifungwa mabao 91, lakini tayari makocha sita wameshatimka.
Ndanda FC imemtimua aliyekuwa kocha mkuu James Kitambi na kocha wa makipa Mohammed Mwarani, Simba imemtimua kocha wa makipa Idd Pazi, Coastal Union imeachana na aliyekuwa kocha mkuu Mkenya Yusuph Chippo na kumwajiri Mkenya James Nandwa huku Yanga wakimtimua Mbrazil Marcio Maximo na msaidizi wake Leonardo Neiva raia wa Brazil.
Aidha, timu ya Stand United ya mjini Shinyanga imeajiri kocha mkuu mpya Mathia Lule ili kuimarisha benchi lake la ufundi kuwasaidia aliyekuwa kocha mkuu Emmanuel Masawe (kaka wa mchezaji bora wa msimu wa 2011/12 wa VPL, Jacob Masawe) na kocha msaidizi Athumani Bilal waliyoipandisha Ligi Kuu timu hiyo ya usukumani.
Yanga, mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, mbali na kuajiri watendaji wengine wapya katika idara za habari, fedha, masoko na katibu mkuu, wamemrejesha Hans van der Pluijm na msaidizi wake Boniface Mkwasa kuchukua nafasi ya Maximo na Neiva lakini ujio wa wataalam hao Jangwani huenda ikawa ni chanzo cha kuharibu wasifu wao (CV) kwani klabu hiyo haina historia nzuri na watendaji inaowaajiri.
yanga
Watendaji walioteuliwa kuunda sekretarieti mpya ya Yanga ni Jonas Tiboroha (katibu mkuu), Jerry Muro, mtangazaji wa zamani wa televisheni za ITV na TBC (Mkuu wa Habari na Mawasiliano), Omari Kaya (Mkuu wa Idara ya Sheria) na Baraka Deusdetit (Mkuu wa Idara ya Fedha).

Kadri ya uelewa wangu kuhusu klabu ya Yanga na soka la Bongo kwa ujumla, ninaamini yaliyomkuta Maximo na watangulizi wengine katika utendaji ya klabu hiyo, yatawafika pia Pluijm, Mkwasa na watendaji wapya waliotangazwa rasmi wiki iliyopita licha ya ukweli kwamba baadhi yao walikuwa na mikataba ya kufanya kazi Jangwani miezi mingi iliyopita.
Kwanza, historia unauhukumu uongozi wa Yanga kwa kutokuwa na uvumilivu kwa makocha na watendaji unaowaajiri. Tangu 1991 vurugu za kutimua ovyo makocha zilipoanza, timu hiyo imepita mikononi mwa makocha 25 ingawa wachache kati yao walifukuzwa na kurudishwa.
Makocha hao waliowahi kuinoa Yanga tangu 1991 ni Syllersaid Mziray, Nzoyisaba Tauzany (Burundi 1993), Tambwe Leya (DRC 1995), Sunday Kayuni (1997), Steve McLennan (Uingereza 1997), Tito Mwaluvanda (1998), Raoul Shungu (DRC 1999), Boniface Mkwasa (2001), Jack Chamangwana (Malawi 2002), Jean Polycarpe Bonganya (DRC 2004), Syllersaid Mziray (2004) na Kenny Mwaisabula (2005).
Wengine ni Chamangwana (Malawi 2006), Milutin Sredojevic ‘Micho’ (Serbia 2007), Razack Ssiwa (Kenya 2007), Chamangwana (Malawi 2007), Dusan Kondic (Serbia 2008), Kostadin Papic (Serbia 2010), Sam Timbe (Uganda 2011), Papic (Serbia 2011), Tom Saintfiet (Ubelgiji 2012), Ernie Brandts (Uholanzi 2012/13), Hans van Der Pluijm (Uholanzi 2014), Máximo (2014) na sasa Pluijm tena.
Kuna kipindi pia makocha wazawa Felix Minziro na Mkwasa waliinoa kwa muda (kipindi cha mpito) wakiwa makocha wakuu.
Licha ya kuwika akiwa na Taifa Stars, Máximo amefukuzwa Yanga baada ya kufungwa dhidi ya Simba, tena katika mechi ya ‘ndondo’. Ameiongoza Yanga katika mechi 14, akishinda 10, sare moja dhidi ya Simba na kupoteza tatu dhidi ya Mtibwa Sugar, Kagera Sugar na Simba.
Pluijm na Mkwasa waliiongoza timu hiyo ya Jangwani katika mechi 19 wakishinda 11, sare sita na kupoteza mbili dhidi ya Al Ahly (1-0 ugenini) na 2-1 dhidi ya Mgambo Shooting. Je, wawili hao wamekuja na jambo gani jipya ambalo Máximo na makocha wengine waliopita (tena baadhi walikuwa maprofesa wa soka) hawakuwa nalo?
Mbali na timua timua ya makocha ambayo inaonesha katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2011, Yanga imenolewa na makocha saba (Timbe, Papic, Saintfiet, Brandts, Pluijm, Maximo na Pluijm tena), klabu hiyo pia imefanya mabadiliko ya makatibu wakuu watatu ndani ya miezi 15, ambao ni Beno Njovu, Lawrence Mwalusako na Selestine Mwesigwa, bila kumsahau Mkenya Patrick Naggi aliyekataliwa na Baraza la Wazee la Yanga.
Pili, Yanga iko katika kipindi kigumu cha kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Juni mwakani badala ya Juni mwaka huu, kinyume cha Katiba ya Yanga na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
8
Binafsi ninaamini ujio wa Máximo Jangwani ulikuwa sehemu ya mikakati ya kujiimarisha kuelekea uchaguzi huo kwani katika mkutano mkuu uliopita (Juni Mosi, mwaka huu), wanachama wa Yanga walionekana kama kushawishika kuuongezea muda wa mwaka mmoja uongozi uliopo madarakani baada ya kutaarifiwa juu ya kurejeshwa nchini kwa mtaalam huyo wa soka.

Kuelekea uchaguzi huo, ninaamini kuwa ni matokeo mazuri tu ya timu yatakayonusuru ajira za Pluijm, Mkwasa na watendaji wengine kwani uongozi uliopo madarakani kwa sasa unaonekana kama bado una nia ya kuendelea kuiongoza Yanga.
Yanga iliyoanzishwa 1935, ina uhakika wa kupata mgawo wa mapato ya mlangoni ambao si chini ya Sh. milioni 100 katika mechi moja tu dhidi ya watani wao wa jadi, Simba.
Bajeti za timu hiyo zinaonesha inatumia si chini ya Sh. milioni 700 katika kipindi cha nusu mwaka. Nani asiyetaka kuongoza timu yenye uhakika wa kuingiza ‘mpunga’ mwingi kama hiyo?
Tatu, mechi za Yanga dhidi ya Simba na Azam FC, pia huenda zikawa shubiri kwa makocha na watendaji wapya wa Yanga kwani historia inaonesha watangulizi wao wengi wamefukuzwa kutokana na matokeo mabovu dhidi ya Simba.
Yanga haina tatizo la wataalam wa ufundi na wengi wa makocha wamekuwa wakitimuliwa kwa sababu mbili kuu; kuwa wakweli kuhusu udhaifu wa Yanga kama ilivyomtokea Mbelgiji Saintfiet aliyekosoa viwanja vya mazoezi na hoteli au kufungwa dhidi ya Simba kama ilivyowatokea Brandts na Máximo baada ya timu kupoteza katika mechi za ‘ndondo’ za ‘Nani Mtani Jembe’.
Nne, kikosi cha Yanga kina udhaifu wa kupwaya kwa safu yake ya ulinzi ambayo ilionesha kuyumba tangu mwishoni mwa msimu uliopita.
Kanavaro
Mabeki wa kati Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wamecheza vizuri kwa muda mrefu lakini wameonekana kama wameanza kuishiwa maarifa, pengine kutokana na umri na kutumika kupita kiasi msimu uliopita wakiwa na kikosi cha Yanga na Taifa Stars bila kupewa muda wa kutosha wa kupumzika.
Kumbuka makosa ya Cannavaro katika mechi yao dhidi ya Kagera Sugar msimu huu (Yanga imepoteza 1-0), rejea makosa ya Yondani dhidi ya Mgambo Shooting (walifungwa 2-1) kisha tafakari kuhusu makosa ya mbadala wao ‘kiraka’ Mbuyu Twite katika mechi dhidi ya Al Ahly (walilala 1-0 ugenini).
Katika mechi saba zilizopita za VPL msimu huu, safu ya ulinzi ya Yanga imeruhusu mabao katika mechi nne.
Hawakufungwa bao katika suluhu dhidi ya Simba na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stand United na 2-0 dhidi ya Mgambo Shooting.
Tano, kumekuwa na tatizo ninaloliona kama tabia za kuwapo kwa uchoyo miongoni mwa wachezaji wa Yanga.
Ni kweli kwamba Yanga ya Máximo imeonekana kama kucheza soka la ovyo na kutokuwa na uhakika wa kupata ushindi, lakini Wanayanga wanapaswa kuelewa kwamba sehemu kubwa ya wachezaji wa Kitanzania hawana weledi.
Ujio wa mara ya pili wa Máximo nchini uliambatana na kutua kwa mshambuliaji Mbrazil Geilson Santos Santana ‘Jaja’ ambaye alifunga mabao mazuri wakati wa mechi za majaribio.
Mabao yake mawili ya video katika ushindi wa 3-0 ambao Yanga iliupata dhidi ya Azam FC katika mechi waliyotwaa Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa Septemba 14, yalithibitisha ni mfumania nyavu wa ukweli.
Hata hivyo, Jaja amefunga bao moja tu katika mechi saba za VPL msimu huu kutokana na kile ambacho Máximo alikisema jijini Dar es Salaam Novemba Mosi kwamba “ubutu wa mshambuliaji husika (Jaja) unatokana na uchoyo wa wachezaji wenzake ndani ya kikosi cha Yanga, hasa viungo”.
Kavumbago
Madai hayo ya Máximo ni mazito lakini binafsi ninaona yana mashiko ikikumbukwa kuwa mshambuliaji Didier Kavumbagu aliyetua Azam FC msimu huu akitokea Yanga, alifunga mabao nane katika mechi 13 za mzunguko wa kwanza wa VPL msimu wa 2012/13 akiwa na kikosi cha Brandts cha Yanga lakini mzunguko wa pili akafunga bao moja tu.

Ni kutokana na mazingira ambayo yalionekana kama Mrundi huyo alikuwa akikomolewa na baadhi ya nyota wa Yanga baada ya kuandikwa kwa kiasi kikubwa na kuvuma kwenye magazeti nchini, Yanga imefunga mabao tisa tu katika mechi saba zilizopita za VPL, madai haya yakiwa ni ya Máximo.
Sababu ya sita ni kujidhatiti kwa timu za VPL msimu huu. Kama nilivyodokeza awali, kabla ya ligi kusimama Novemba 9 kupisha usajili wa dirisha dogo, zilikuwa zimechezwa mechi 49 zilizozaa mabao 91, huku 50 yakifungwa na timu mwenyeji (uwanja wa nyumbani) ilhali timu ngeni zimefunga mabao 41, ikiwa ni wastani wa goli 1.86 kwa mechi.
Mpaka sasa wanaoongoza kwa mabao Kavumbagu, Rama Salim (Coastal), Dan Mrwanda (Polisi/Yanga) na Ame Alli Amour (Mtibwa) wana mabao manne kila mmoja.
Hadi mechi zote 49 za raundi saba za mwanzo za VPL msimu uliopita yalikuwa yamefungwa mabao 101 ikiwa ni wastani wa mabao mawili kwa kila mechi.
Mshambuliaji Mrundi Amissi Tambwe (Simba/Yanga) alikuwa amefunga mabao nane peke yake hadi hatua hiyo licha ya kukosa mechi ya kwanza dhidi ya Rhino Rangers, mabao ambayo ni sawa na mabao yote ya Azam FC katika mechi zote saba msimu huu.
ngassa-goal
Mfungaji bora wa Yanga msimu uliopita wa VPL na Klabu Bingwa Afrika, Mrisho Ngasa hajafunga bao hata moja msimu huu wakati msimu uliopita licha ya kukosa mechi tano za mwanzo kutumikia adhabu, alifanikiwa kufunga mabao 13 na kutoa pasi za mwisho 17 VPL akifunga pia mabao sita katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Hali haikuwa shwari pia kwa mshambuliaji Hamis Kiiza aliyetemwa. Mganda huyo msimu uliopita aliifunga Yanga mabao 12 akimfuata Ngasa na hadi raundi ya saba alikuwa na mabao mawili.
Mfungaji bora wa wa msimu 2012/13, Kipre Tchetche wa Azam FC aliyefunga mabao 17, amefunga bao moja tu katika mechi tano kati ya saba alizopangwa msimu huu katika kikosi cha Mcameroon Joseph Omog cha Azam FC.
Kama hiyo haitoshi, Mbeya City ambayo inanolewa na kocha bora wa msimu uliopita, Juma Mwambusi, imefunga mabao mawili tu (bao moja limetokana na pigo la penalti) katika mechi zote saba msimu huu ikiwa na mfungaji bora wa Oljoro JKT msimu wa 2012./13, Paul Nonga na mfungaji bora wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) msimu wa 2012/13, Saad Kipanga (alifunga mabao 12 katika mechi 14 na kuipandisha VPL Rhino Rangers ya Tabora).
Mbeya City pia wana mfungaji bora wa Kagera Sugar, Themi Felix.
Kwa kifupi mpaka sasa vinara Mtibwa Sugar wamefunga mabao 10 na kufungwa matatu, Azam FC (8-4), Yanga (9-5), Coastal (9-7), Kagera Sugar (6-4), JKT Ruvu (7-7), Simba (7-6), Polisi Morogoro (6-7), Mgambo (3-6), Stand (5-9), Ruvu Shooting (4-8), Prisons (6-7), Ndanda (8-12) na Mbeya City (5-2).

Takwimu hizi zinaonesha kuwa timu zimejidhatiti vilivyo msimu huu hivyo haitakuwa rahisi kwa Yanga kupata mafanikio licha ya kumfungashia virago Máximo na kuleta wataalam wapya katika benchi la ufundi na sekretarieti.
Saba na mwisho ni usajili mbovu unaofanywa na klabu nyingi nchini bila kuzingatia misingi ya weledi. Yanga imefanya usajili kwa kuongeza, kuwatema na kuwatoa kwa mkopo baadhi ya nyota.
Hata hivyo, usajili uliofanyika Yanga dirisha dogo umefanywa kwa usimamizi wa Máximo aliyetimuliwa.
Kwa msingi huo, Pluijm na Mkwasa wanafundisha wachezaji waliosajiliwa na Máximo, ambaye uongozi wa Yanga umeona hafai.
Je, wawili hawa wataipa vipi mafanikio timu hiyo ya Jangwani kupitia kwa wachezaji waliosajiliwa na kocha aliyefeli? Pengine, Mliberia Kpah Sherman, Mbrazil Andrey Coutinho, Mrundi Tambwe na wazawa Mrwanda na kipa Alphonce Majogo hawajasajiliwa kwa pendekezo la Máximo.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video