Friday, December 5, 2014

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Phiri (kushoto) akiwanoa vijana wake

KOCHA mkuu wa Simba sc, Patrick Phiri amesema kikosi chake kinazidi kuimarika kutokana na mazoezi ya nguvu wanayoendelea kuyafanya kwa sasa kujiandaa na raundi ya nane ya ligi kuu soka Tanzania bara na mechi ya Nani Mtani Jembe 2.
Akizungumza katika mazoezi ya Simba yanayoendelea kufanyika uwanja wa JKT Mbweni jijini Dar es salaam, Phiri alisema baada ya kutoka mazoezi ya Gmy ameona mabadiliko ya vijana wake na wanatia matumaini kuelekea mechi zijazo.


Mzambia huyo aliongeza kuwa lengo ni kuhakikisha idara zote zinakuwa na nguvu ya kutosha, lakini anaangalia zaidi sehemu ya ushambuliaji kwani mpaka sasa timu hiyo haijafunga mabao mengi.

“Kusajiliwa kwa Sserunkuma (Danny) ni jambo nzuri sana. Nimemuona mara kadhaa akiichezea timu yake ya Taifa (Uganda). Ni mchezaji mahiri. Wakikaa na Okwi (Emmanuel) na Tambwe (Amiss)  nadhani tutakuwa na safu yenye ubora”.Alisema Phiri.

Kuelekea mechi ya nani Mtani Jembe itakayopigwa Desemba 13 mwaka huu, Phiri alisema maandalizi yanakwenda vizuri na anafurahi kukutana na Yanga.

“Itakuwa mechi nzuri. Yanga ni wapinzani wetu wakubwa na timu kubwa nchini, tunaendelea kujipanga na tunaamini kuibuka na ushindi”.

“Nawashukuru sana mashabiki wetu, wamekuwa nasi kwa wakati wote. Sasa ni muda wa kuwafurahisha”.

Simba leo inatarajia kucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya The Express ya Uganda katika uwanja wa Taifa na jumapili itakipiga na Mtibwa Sugar katika uwanja huo.


Baada ya mechi hizo, Mnyama anatarajia kuweka mawindo yake visiwani Zanzibar kuitafuta mwarobaini Yanga .

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video