Monday, December 29, 2014

IVO
KIPA namba moja wa Simba sc, Ivo Philip Mapunda ametangaza rasmi kuondoka Simba kutokana na muendelezo wa shutuma juu yake kuwa anaihujumu timu.
Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Ivo tayari amemuambia kocha wake mkuu Patrick Phiri asimpange tena katika mechi za ligi kuu soka Tanzania bara.
Ivo alifungwa bao rahisi ijumaa ya wiki iliyopita katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambapo  Simba ilifungwa goli 1-0.
Simba imeshaanza mazoezi leo asubuhi katika Gym ya Chang’ombe Dar es salaam na mchana huu inaingia kambini katika Hoteli ya Upland iliyopo maeneo ya Changanyikeni jijini Dar.
Kikosi hicho chini ya kocha Phiri kitakuwa kinafanya mazoezi yake katika uwanja wa Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) mpaka siku ya ijumaa ambapo kitasafiri kwenda Tanga tayari kwa mechi dhidi ya Mgambo JKT Januari 4 mwaka huu uwanja wa CCM Mkwakwani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video