Tuesday, December 2, 2014

MSHAMBULIAJI hatari wa Polisi Morogoro, Danny David Mrwanda amakiri kumaliza mazungumzo na viongozi wa Simba juu ya yeye kujiunga na timu hiyo wakati huu wa dirisha dogo la usajili.

Mrwanda amesema makubaliano yamefikiwa na imebaki kwa upande wa Simba kutekeleza matakwa yake ili ajiunge na wekundu hao wa Msimbazi.

Nyota huyo wa zamani wa Taifa Stars na Simba tayari yupo jijini Dar es salaam kusikilizia mpango huo na kama mambo hayataenda sawa anatarajia kutua nchini Vietnam kucheza soka la Kulipwa.

“Kwasasa nipo hapa Dar es salaam, kuna mambo nayamalizia. Kweli nimezungumza na Simba, kilichobaki ni wao kutekeleza makubaliano”. Alisema Mrwanda alipohojiwa na mtandao huu.

Mrwanda ni miongoni mwa wachezaji waliopendekezwa na kocha mkuu wa Simba, Patrick Phiri katika ripoti yake baada ya mechi saba za ligi kuu Tanzania bara.

Katika mechi sita zilizopita, Simba ilipata sare zote na kushinda moja.


Simba imeanza mazoezi ya Gym na uwanjani maeneo ya Chang’ombe jijini Dar es salaam.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video