Tuesday, December 2, 2014

Cranes
KAMPALA, Uganda
Waziri wa Michezo wa Uganda Charles Bakkabulindi amesema serikali ya nchi hiyo itajitwisha majukumu ya kuteua kocha mkuu wa timu ya taifa hilo ‘The Cranes’ ili kuongeza ubora wa timu hiyo katika michuano ya kimataifa.
Uthibitisho huo wa Waziri unakuja baada ya kuripotiwa na New Vision, mara tu baada ya Uganda kushindwa kufuzu fainali zijazo za Mataifa ya Afrika kwa mara ya tatu mfululizo katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

“Serikali itaandaa utaratibu wa kuzingatia katika kuhakikisha timu inakuwa tayari kwa michuano ijayo, amekaririwa Waziri huyo na New Vision.
Mkataba wa kocha wa sasa Milutin ‘Micho’ Sredojevic na The Cranes utafikia tamati Mei 2015 na tayari amehusishwa kuwa na mpango wa kutimkia Afrika Kusini kuinoa Timu ya Free State Stars.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video