Tuesday, December 2, 2014

Imbem
Mshambuliaji Itubu Imbem wa Coastal Union amesema Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ina ushindani mkali ikilinganishwa na Ligi Kuu ya Kenya (KPL).
Imbem aliyewahi kucheza katika vikosi vya klabu za Kenya, AFC Leopards, Tusker FC na mabingwa wa KPL Gor Mahia kabla ya kutimkia Al Hilal ya Yemen na baadaye kutua Coastal Union, amesema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya VPL na KPL.

“Nimecheza katika ligi hizi mbili na ninachoweza kukisema ligi ya Tanzania ni ngumu kuliko ya Kenya. Hii ya Tanzania ina ushindani mkubwa na timu zote katika ligi hii ni nzuri. Kenya tofauti iliyopo kati ya timu zilizopo kileleni na timu nyingine ni kubwa lakini kwa Tanzania hali hiyo haipo na ndiyo maana kila wiki ya mashindano unaona timu iliyoko kileleni inapoteza dhidi ya klabu inayochukuliwa kama ‘timu ndogo’.
“Ushindani katika ligi ni mkubwa na hiyo ndiyo sababu kubwa tunapewa changamoto ya kuhakikisha tunakuwa vizuri katika kila mechi,” amesema Imbem.
Imbem leo ameripotiwa na mtandao wa futaa.com kwamba kwa sasa anakipiga katika michuano ya Koth Biro nchini Kenya baada ya VPL kusimama kwa wiki sababu kupisha usajili wa dirisha dogo na michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kufanyika mwezi huu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video