Wednesday, December 3, 2014

SAM_3548
BEKI anayeaminiwa kwa sasa na kocha wa Simba sc, Patrick Phiri, Hassan Isihaka amesema kuwa  kujiamini, kujituma na kuwa na subira ndio siri ya mafanikio yake ya sasa.
Isahaka amesema amepita mikononi mwa makocha tofauti Simba SC, lakini amekuja kuaminiwa na kocha wa sasa.

“Nimehangaika sana, nakumbuka kuna wakati nilitolewa kwa mkopo kwenda Africa Lyon. Kocha kama Logarusic (Zdravko) hakuniamini kabisa. Alivyokuja Phiri nikajiamini na kuonesha kile nilichokuwa nacho”. Alisema Isihaka.

“Loga hakuwaamini vijana, lakini Phiri ni kocha anayetutia moyo na kutufanya tucheze mpira kwa kujiamini”

Beki huyo ambaye amecheza mechi zote saba za ligi kuu Tanzania bara aliongeza kuwa anajitahidi kukwepa kufanya makosa yasiyokuwa ya lazima ingawa mpira wa miguu ni mchezo wa makosa.

Aidha alisema kuwa malengo yake ni makubwa na anataka kuisadia kwanza Simba msimu huu halafu mambo mengine yatafuata.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video