Wednesday, December 3, 2014

SAM_3562
Cholo akiwa Gym kufanya mazoezi

NAHODHA wa Simba, Masoud Nassor ‘Cholo’ kwasasa yuko fiti kucheza mechi ya aina yoyote.
Daktari wa Simba, Yassin Gembe ameuambia mtandao huu kuwa afya ya Cholo ambaye amerithiwa unahodha na Joseph Owino imeimarika kwa asilimia mia moja kufuatia kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara.

“Cholo yuko fiti kucheza hata kesho. Hivi tunavyozungumza alikuwa kambi ya timu ya taifa ya Zanzibar kujiandaa na michuano ya  CECAFA Challenge”. Alisema Gembe.

SAM_3546
Baba Ubaya akiwa mazoezini

Daktrai huyo aliongeza kuwa beki wa kushoto wa klabu hiyo ambaye amesumbuliwa na majeruhi kwa muda mrefu sasa, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ naye amepona majeraha yake.

“Issa (Rashid) yuko fiti pia. Ameanza mazoezi na yuko tayari kwa mechi”. Alisema Gembe.

Kuhusu Paul Kiongera, Gembe alisema kuwa mshambuliaji huyo raia wa Kenya amemaliza muda wake wa mapumziko, lakini bado ni majeruhi na hawezi kusema atarudi uwanjani siku gani.

“Kiongera hali yake bado kabisa, kwahiyo siwezi kusema ni lini atakuwa tayari kucheza”. Alisema Gembe.


Wekundu wa Msimbazi Simba wanaendelea na mazoezi mara moja kwa siku ambapo wanaanzia Gym na kumalizia katika uwanja wa TCC Sigara Chang’ombe Dar es salaam.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video