Sunday, December 14, 2014

BEKI wa kulia wa Simba, Masoud Nassor ‘Cholo’ amesema Simba ni timu kubwa hivyo kuona mabadiliko ya wachezaji ni suala la kawaida.
P 1 (1)
Cholo kulia
Cholo ambaye alianza katika kikosi cha Simba kilichoshinda mabao 2-0 dhidi ya Yanga jana alisema amefurahishwa na ujio wa wachezaji wapya kwani wameongeza chachu ya ushindani.
“Timu imecheza vizuri na kila mtu alijituma sana. Wachezaji wapya (Juku Musheed, Simon Sserunkuma, Danny Sserunkuma) ni watu waliongeza ushindani na ubora wa kikosi”. Alisema Cholo.
Aidha, beki huyo aliyesumbuliwa na majeruhi ya muda mrefu alisema sasa yuko fiti na anajituma kurudisha kiwango chake.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video