Tuesday, December 30, 2014


Sitti Mtemvu na Ludenga
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam

Kitendo cha waandaaji wa Miss Tanzania kuwasilisha hundi feki ya mamilioni ya shilingi katika Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kusaka kibali cha shindano hilo ni miongoni mwa sababu sita zilizosababisha kufungwa kwa shindano hilo kubwa nchini.

Katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za makao makuu ya Basata jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Godfrey Mngereza ametangaza rasmi kulifunga shindano hilo kwa miaka miwili kuanzia 2015 hadi 2016.

"Hundi ya malipo ya kibali cha Sh. 2,000,000 (Sh. milioni mbili) iliyoletwa Basata ilikuwa kifawi (Fake Cheque)," Mngereza amesema wakati akieleza sababu ya sita ya kufungwa kwa shindano hilo kubwa katika fani ya urembo nchini.

Awali kiongozi huyo wa serikali amesema mchakato mzima wa kufunga shindano hilo umejikita katika sababu nyingine tano ambazo ni hatua ya uongozi wa LINO International Agency (waandaaji wa Miss Tanzania) kushindwa kujibu barua mbalimbali za kuwakumbusha kufuata taratibu za uendeshaji wa mashindano ya urembo ambazo baraza lilikuwa linawaandikia.

Kushindwa kulipa gharama za kibali cha uendeshaji wa shughuli za sanaa za mwaka 2014 huku pia ikibainika kuwa mawakala waliohusika katika kuendesha shindano hilo hawakusajiliwa kwa mujibu wa Kanuni Na. 9(a) "mawakala kusajiliwa na Basata".

Kushindwa kuwasilisha zawadi za washindi siku 14 kabla ya fainali kinyume cha Kifungu cha 10(a) na (b) cha Kanuni za LINO "kuwasilisha zawadi za washindi siku 14 kabla ya fainali kwa mamlaka ya serikali inayohusika na masuala ya sanaa."

"Pia mikataba ya washiriki haikuwasilishwa kwa wakati," amesema zaidi Mngereza.

Amesema Basata imefikia uamuzi huo kutokana mchakato wa uendeshaji wa shindano la Miss Tanzania ulivyokwenda katika msimu wa 2014 ambao wamegundua na kujiridhisha kuwa uongozi wa LINO International Agency umekiuka Kanuni za Uendeshaji na Kanuni na taratibu za baraza hilo zinazoongoza uendeshaji wa matukio ya sanaa.

Aliyekuwa mshindi wa taji la Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu alilazimika kulivua na kukabidhiwa kwa mshindi wa pili Lilian Kamazima baada ya Sitti kukumbwa na kashfa ya kudanganya umri.

Shindano hilo limefungwa ikiwa ni siku chache baada ya kurejea nchini kwa Miss Tanzania wa mwaka jana Happiness Watimanywa aliyekuwa nchini Uingereza akiiwakilisha Tanzania katika shindano la urembo la dunia (Miss World).

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video