Tuesday, November 4, 2014

Kikosi cha timu ya Young Africans tayari kimesharejea jijini Dar es salaam kutok kanda ya Ziwa ambapo kilicheza michezo miwili ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Stand United ya mjini Shinyanga na Kagera Sugar ya mjini Bukoba na kujikusanyia pointi tatu kati ya pointi sita.
Mara baada ya kurejea jijini Dar es salaam kocha Marcio Maximo alitoa mapumziko ya siku moja kwa wachezaji wake kabla ya leo jioni kuanza mazoezi ya Gym eneo la Posta kuweka mili safi lna kesho kuendelea na mazoezi asubuhi katika Uwanja wa shule ya Sekondari Loyola
Akizungumzia mechi mbili zilizochezwa kanda yta ziwa, Maximo amesema walijitahid kucheza na kusaka ushindi kwa nguvu zote lakini pia timu walizocheza nazo zilikua nyumbani na kupambana kuhakikisha nazo hateztipotezi mchezo nyumbani.
"Tumepata pointi tatu kati ya sita katika michezo miwili ya ugenini kanda ya ziwa, mechi zilikuwa ngumu wenyeji waliicheza kwa nguvu kusaka pointi viwanja vya nyumbani hali iliyotupelekea kupata ushindi wa mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja"alisema Maximo
Aidha Maximo amesema mchezo dhidi ya Kagera Sugar mwamuzi alishindwa kulimudu pambano, mechi haikuchezwa kwa dakika 90 kutoka na kusimama kwa zaidi ya dakika 10 kutokana na wachezaji wa Kagera kupoteza muda, lakini katika hali ya kustajabisha waliongeza dakika tatu tu ambazo pia mchezaji wa wakata miwa alitumia kutibiwa ndani ya Uwanja.
Kiukweli kuna wakati mgumu sana kwa soka la Tanzania kufika hatua za juu, waamuzi wamekua na makosa mengi ambayo yanaonekana dhahiri, lakini pia Uwanja wa Kaitaba haufai kwa kuchezewa kwa Ligi kuu kwani mbovu kupita kiasi, kwani pia unatumka kwa shuguli za mashindano ya Pikipiki na maonyesho mbalimbali.
Young Africans inatarajia kucheza na Mgambo JKT siku ya jumamosi kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijni Dar es salaam mchezo ambao kocha Maximo amesema ni muhimu kupata pointi tatu ili kurejea katika nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video