Monday, November 17, 2014


Baada ya kukamilika kwa raundi ya saba, Mtibwa Sugar wapo kileleni kwa pointi 15 wakifuatiwa na Yanga katika nafasi ya pili wakijikusanyia pointi 13.

Mabingwa watetezi Azam fc wapo nafasi ya tatu wakijikusanyia pointi 13 sawa na Yanga, lakini wanazidiwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Timu ya Ndanda fc inaongozwa kwa kufungwa mabao mengi kwani mpaka sasa nyavu zake zimetikishwa mara 12.

Vinara Mtibwa Sugar ndio timu pekee iliyofungwa magoli machache ambapo nyavu zake zimetikishwa mara tatu.

Timu zinazofuatia kufungwa mabao machache ni Azam fc na Kagera Sugar ambazo zimefungwa mabao manne.

Timu ya Mtibwa Sugar inaongoza kwa kufunga mabao mengi ambapo imetia kambani magoli 10, ikifuatiwa na Yanga, Coastal Union zilizofunga mabao tisa.

Simba ni timu pekee inayoongoza kutoka sare ambapo imetoka sare mara sita mfululizo.

Lakini Mnyama na Mtibwa Sugar ndio timu pekee ambazo hazijafungwa mpaka sasa.


Timu za Mgambo JKT, Mbeya City fc na Ruvu Shooting zinaongoza kwa kupoteza mechi nyingi ambapo zimefungwa katika michezo minne. Ligi kuu Tanzania bara itaanza kutimua vumbi tena Desemba 26 mwaka huu na ratiba nzima iko hivi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video