
Mtanange mwingine ilioweka rekodi ulikuwa baina ya
Stand United dhidi ya Mbeya City fc katika dimba la CCM kambarage mkoani
Shinyanga.
Stand waliweka rekodi ya kushinda kwa mara ya kwanza
ligi kuu wakiwa uwanja wao wa nyumbani.
Septemba 20 mwaka huu walianza ligi kwa kucheza
mechi ya kwanza nyumbani na kutandikwa mabao 4-1 dhidi ya Ndanda fc.
Mechi ya pili nyumbani walicheza Oktoba 25 mwaka huu na kufungwa mabao 3-0 na
Dar Young Africans.
Mechi ya tatu ya nyumbani walikabiliana na Tanzania
Prisons Novemba 11 mwaka huu na kutoka sare ya bao 1-1.
Stand wakafufukia kwa Mbeya City fc kwa kuichapa bao
1-0 katika uwanja wao.
0 comments:
Post a Comment