Wakati Azam
wakicheka uwanja wa Taifa, Dar Young Africans walikuwa na kibarua kizito
kuwakabili maafande wa Mgambo JKT Katika dimba la Taifa, Dar es salaam.
Mechi hiyo
iliyotawaliwa na rafu nyingi ilimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao
2-0.
Wachezaji
wa timu zote walioneshana ubabe wa hapa na pale, lakini mara kadhaa mwamuzi
Ngole Mwangole kutoka Mbeya alipeta.
Hata hivyo,
Mgambo walilazimika kucheza pungufu kwa dakika 38 baada ya mchezaji wao Salum
Hamis Kipaga kuoneshwa kadi nyekundu kufuatia kumpiga kiwiko Mrisho Ngassa.
Naye Mbuyu
Twite alimpiga teke Fuluzulu Maganga wa Mgambo akilipiza kisasi kufuatia
kufanyiwa madhambi, lakini mwamuzi Ngole Mwangole kutoka Mbeya alimuonesha kadi
ya njano.
Kitendo
hicho kilizua utata ambapo mashabiki, wachambuzi na makocha wa mpira walidai
kuwa Twite alistahili kadi nyekundu.
Mbali na
matukio hayo, Malimi Busungu alijikuta akioneshwa kadi ya njano akidaiwa
kujiangusha, lakini picha za marudio zilionesha dhihiri kuwa aliangushwa na beki wa Yanga.
Licha ya
kuwa pungufu, Mgambo JKT walishambulia lango la Yanga, lakini kipa Deo Munish
alijitahidi kuonesha umahiri wake kwenye milingoti mitatu.
Nao Yanga
walijizatiti kuhakikisha wanapata magoli na katika dakika ya 73, Saimon Msuva akitokea
benchi aliandika bao la kuongoza akimalizia mpira mrefu wa Mbutu Twite.
Dakika za
majeruhi, Msuva aliandika bao la pili akimalizia mpira uliookolewa na beki wa
Mgambo kutokana na purukushani za Hassan Dilunga.
Ilionekana
Dilunga amemfanyia madhambi mlinda mlango wa Mgambo, lakini haikumzuia mwamuzi
kukubali goli hilo.
0 comments:
Post a Comment