Monday, November 10, 2014

JIJINI Dar es salaam kulikuwa na mchezo mkali baina ya Simba na Ruvu Shootings ya Pwani.

Mechi hii ilivuta hisia za mashabiki wengi kutokana na mfululizo wa matokeo ya sare sita kwa wekundu wa Msimbazi Simba.
Mnyama Simba ilianza kwa kasi kulisakama lango la Ruvu Shootings wakisaka bao la kuongoza.

Mara kadhaa Amissi Tambwe, Emannuel Okwi na kiungo Said Ndemla walikosa nafasi nzuri za kuandika magoli.

Naye beki wa kati Joseph Owino alikuwa anapanda kuongeza kasi ya mashambulizi, lakini dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Kipindi cha pili Tambwe na Okwi waliokenaka kuwa na kasi kubwa wakisaka goli, lakini mabeki wa Ruvu Shooting walikuwa makini kuokoa.

Simba hawakukata tamaa hata kidogo kwani walijua wazi kuwa mashabiki wa timu hiyo wana hamu ya ushindi.

Mashabiki wachache waliokaa jukwaa la Yanga waliendelea kuwakebehi wachezaji wa Simba na mashabiki wake.

Lakini Elias Maguri aliyetokea benchi aliwachachafya mabeki wa Ruvu Shootings na katika dakika ya 77 aliingia eneo la hatari na kupiga mpira uliokolewa na kipa wa Shootings na Emmanuel Okwi alimalizia na kuwainua vitini mashabiki wao.
Katika mechi sita za mwanzo, Simba walikuwa wanafunga mabao katika kipindi cha kwanza na kurudishwa kipindi cha pili.

Walitangulia kwa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union, lakini yakasawazishwa kipindi cha pili.

Walitangulia kwa bao 1-0 dhidi ya Polisi Morogoro, lakini likasawazishwa kipindi cha pili. Walitangulia kwa bao 1-0 dhidi ya Stand United, likasawazishwa kipindi cha pili.

Mechi ya watani wa jadi dhidi ya Yanga hawakufungana, lakini katika mechi dhidi ya Prisons walitangulia kwa bao 1-0, lakini likasawazisha na katika mechi na Mtibwa walitangulia bao 1-0, likasawazishwa kipindi cha pili.


Mechi ya mwishoni mwa wiki hawakufunga goli kipindi cha kwanza na kundi la UKAWA liliingia uwanjani na kuonesha kidole kimoja juu wakimaanisha timu inashinda 1-0 na ikatokea hivyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video