
Mechi nyingine iliyoweka rekodi mpaka kufikia raundi
ya saba ni ile ya Mgambo JKT dhidi ya Mbeya City fc iliyopigwa uwanja wa CCM
Mkwakwani Tanga oktoba 3 mwaka huu.
Awali mechi hii ilipangwa kuchezwa Oktoba 2 mwaka
huu, lakini kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Tanga, uliahirishwa kufuatia
uwanja kujaa maji.
Mbeya City fc waliokuwa na hamu ya kushinda baada ya
kufungwa mechi mbili mfululizo, bao 1-0 dhidi ya Azam fc na mabao 2-0 na Mtibwa
Sugar uwanja wa Sokoine walijikuta wakifungwa mabao 2-1 na Mgambo.
Wakiendelea kujiuliza nini kimetokea, wakajikuta
wakifungwa tena 1-0 na Stand United, Oktoba 8 mwaka huu uwanja wa CCM Kambarage
Shinyanga.
Rekodi iliyowekwa na Mbeya City msimu huu ni
kufungwa mechi nne mfululizo na kushika mkia katika msimamo wa ligi kuu
ikijikusanyia pointi tano tu.
Pia ni timu pekee iliyofunga mabao mawili tu, tena
moja la penati ya Deogratius Julius kwenye mechi dhidi ya Coastal Union
iliyochezwa septemba 27 mwaka huu uwanja wa Sokoine Mbeya.
Deus Kaseke aliifungia bao la pili msimu huu katika
kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mgambo JKT.
0 comments:
Post a Comment