
KATIKA uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga mzimu wa vipigo umeendelea kuwakumba wagonga
nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc kufuatia kutandikwa bao 1-0 na wenyeji, Stand
United.
Kabla ya
mechi hiyo, makocha wa timu zote mbili walizungumzia kipute hich
Mechi
ilianza kwa timu zote kusaka bao, lakini Stand United walifanikisha ndoto yao
ya kutikisa nayvu kupitia kwa Daniel Barnabas.
Huo ulikuwa
ushindi wa kwanza wa nyumbani kwa Stand United kwani tangu kuanza kwa ligi kuu
hawakuwahi kushindi katika uwanja wao.
Walianza
kwa kuchapwa mabao 4-1 na Ndanda fc,
wakatandikwa mabao 3-0 na Yanga na kutoka sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons
na hatimaye wamejikuta wakifufukia kwa Mbeya City.
Hata hivyo,
Stand United wangeshinda zaidi ya bao moja kwani walipoteza Mkwaju wa penati.
Hali
imezidi kuwa mbaya kwa kocha Juma Mwambusi kwani ni mechi ya nne mfufulizo
anapokea kichapo.
Awali alitandikwa
bao 1-0 na Azam fc katika uwanja wa Sokoine, akapigwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar
katika uwanja huo, alisafiri mpaka CCM Mkwakwani Tanga ambapo alikula kipigo cha
2-1 kutoka kwa Mgambo JKT.
0 comments:
Post a Comment