
MECHI ya Azam fc dhidi ya JKT Ruvu iliyochezwa Oktoba 25 mwaka huu uwanja wa Azam Complex, uliopo
Chamazi jijini Dar es salaam alivunja rekodi.
Bao pekee la Samuel Kamuntu lilitosha kuipa ushindi
wa bao 1-0 JKT Ruvu inayonolewa na Fred Felix Minziro.
Azam fc ilifungwa kwa mara ya kwanza baada ya kucheza
mechi 38 za ligi kuu Tanzania bara bila kufungwa.
Msimu uliopita Azam fc walichukua ubingwa bila
kufungwa katika mechi zao 26 za ligi kuu.
Mzunguko wa kwanza walikuwa chini ya kocha
Muingereza Sterwart John Hall na mzunguko wa pili waliongozwa na kocha wa sasa
Mcameroon Joseph Marius Omog.
Msimu huu wameweka rekodi ya kufungwa mara mbili mfululizo baada ya kucheza
mitanange 38 bila kufungwa.
Waliadabishwa bao 1-0
na Ndanda fc na kujikuta wakitibua kabisa rekodi yao murua
0 comments:
Post a Comment