
MTIBWA SUGAR na Yanga walichuana septemba 20 mwaka huu uwanja wa
Jamhuri Mkoani Morogoro.
Mashabiki lukuki walijitokeza kushuhudia majeshi ya
Yanga yakiongozwa na Wabrazil wawili katika benchi la ufundi yaana Marcio
Maximo na msaidizi wake Leonardo Neiva na mshambuliaji Geilson Santos Santana
‘Jaja’.
Mbrazil mwingine ambaye ni kiungo mshambuliaji, Andrey Coutinho alikuwa majeruhi kwa wakati
huo.
Jaja aliingia uwanjani akiwa na kumbukumbu ya kufunga
mabao mawili peke yake katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Yanga ikiicharaza Azam fc mabao 3-0.
Watu walifurika katika mechi hiyo, na rekodi
aliyowekwa na Jaja nchini ni kukosa penati katika mchezo wake wa kwanza wa ligi
kuu.
Naye Maximo aliweka rekodi ya kufungwa katika mechi
yake ya kwanza akifundisha ngazi ya klabu nchini.
0 comments:
Post a Comment