Hassan Isihaka (kulia). Picha na Bin Zubeiry
BEKI anayezidi kukonga nyoyo za Wanamsimbazi,
Hassan Isihaka amesema matokeo ya sare wanayozidi kupata yanawaumiza mno na
hawaelewi kwanini inakuwa hivyo.
Isihaka aliongeza kuwa kwa wakati wote wachezaji
wamekuwa tayari kucheza, wanajituma, wanafunga magoli, lakini yanarudi kirahisi
tu.
“Unajua hata sisi hatuelewi kwanini inakuwa hivi.
Tunafanya vizuri, lakini tunaishia kupata sare. Nakwambia inatuuma sana na
hatuelewi kwanini inakuwa hivi”. Alisema Isihaka.
Mlinzi huyo mahiri ambaye alifanya makosa mechi
iliyopita na kuwapa mwanya Mtibwa Sugar kusawazisha goli alisema kuwa wakati wote
anajitahidi kutekeleza majukumu yake na kukwepa kufanya makosa, lakini mpira wa
miguu ni mchezo wa makosa.
Pia alimsifu kocha wa Simba Patrick Phiri kuwa ni
kama baba mlezi.
“Kocha Phiri ni mzuri sana. Anaishi na sisi kama
Baba Mlezi. Anajua kuelekeza, ana mbinu nzuri, uongozi ungempa muda zaidi,
naamini tutafanikiwa kufanya vizuri zaidi”. Alisema Isihaka.
0 comments:
Post a Comment