Tuesday, November 18, 2014

Na Mwandishi Wetu
KIKOSI cha timu ya Friends Rangers, kesho kinajitupa  kwenye Uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga, kuvaana  na timu ya African Sports, katika mchezo wa ligi daraja la kwanza.
Mchezo huo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa  ligi, ambapo kila timu inahitaji kupata pointi tatu iweze  kuanza vizuri mzunguko wa pili.
Ofisa Habari wa klabu hiyo, Asha Kigundula, alisema  kuwa tayari kikosi hicho kipo mkoani Tanga kwa ajili ya  mchezo huo.
Kigundula alisema kikosi chao kinaingia uwanjani  kikiwa na taadhari kubwa ya kutopoteza kwa sababu ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mechi zaidi ya kutoka sare.
Alisema kuwa ana amini kila kitu kinawezekana hata ushindi ni muhimu na ikipata ushindi inaweza kurudi katika nafasi ya kuongoza.
Kigundula alisema kuwa kikosi chao chini ya kocha wao  Ally Yusuph ‘Tigana, kina ari kuwa ya kupata ushindi, licha ya wachezaji wake wawili wa kikosi cha kwanza
kutoenda mkoani Tanga.Alisema wachezaji hao ambao ni Almas Mkinda, alipewa kadi nyekundu katika mchezo wao uliyopita dhidi ya Kimondo na Eliute Justine ni majeruhi.
Alisema kuwa kikosi kicho ambapo kimecheza mechi mbili za ugenini na kupata pointi nne katika mechi mbili, wana amini na huko kitafanya vizuri.
Kigundula alisema wanautambua ubora wa timu pinzani, lakini nao wamejipanga kufanya vizuri nakuibuka na ushindi ili waendelee na malengo yao ya kupanda ligi kuu msimu ujao.
Friends Rangers inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 20, huku Majimaji ikiongoza kwa kuwa na pointi 21, hivyo ikishinda itakuwa inaendelea vyema na safari yake ya kupanda daraja.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video