
Picha na Bin Zubeiry
Mkoani
Morogoro katika uwanja wa Jamhuri, timu ya soka ya Polisi ilitamba kwa kuichapa
Tanzania Prisons bao 1-0.
Timu zote
mbili zilianza mchezo kwa kushambuliana, lakini washambuliaji wa pande zote
walikosa umakini.
Hadi dakika
45 za kipindi cha kwanza zinakamilika, hakuna timu iliyofanikiwa kutikisa nyavu
za mpinzani wake.
Katika kipindi
hicho timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji kuimarisha vikosi vyao.
Mabadiliko
hayo yaliisaidia Polisi iliyojipatia bao
pekee la ushindi katika dakika ya 74, mfungaji akiwa Danny David Mrwanda .
Baada ya
mechi kumalizika, manahodha wa timu zote walizungumzia mechi hiyo.
0 comments:
Post a Comment