
MLINDA mlango namba mbili wa Simba sc, Hussein
Sharrif ‘Casilas’ ameanza mazoezi leo baada ya kutoa nyuzi alizoshonwa kwenye
ugoko kufuatia kuumia katika mazoezi ya Mnyama yaliyofanyika nchini Afrika
kusini mwezi uliopita.
Casillas ameanza mazoezi ya Gym na kukimbia mchangani
baada ya kufungua nyuzi za chuma
alizoshonwa.
Kipa huyo bora wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu
uliopita anaanza mazoezi ya peke yake na anaamini Mungu atamjaalia afya njema
ili arudi uwanjani.
Casillas aliumia Oktoba 11 mwaka huu, Simba
ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Orland Pirates nchini Afrika kusini iliyomalizika kwa suluhu
ya bila kufungana.
Kipa huyo aligongwa ugoko kwa njuma za chuma na
mshambuliaji wa miamba hiyo ya Afrika kusini.
Kwasasa Simba inamtegemea zaidi kipa namba tatu,
Peter Manyika Jr kwani hata kipa namba moja Ivo Mapunda hajawa fiti kwa asilimia
100.
Wakati huo huo kuna taarifa kuwa Simba inataka
kumrudisha kipa wake wa zamani anayecheza Yanga, Juma Kaseja katika kipindi
hiki cha dirisha dogo la usajili.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia
Hans Poppe alisema katikati ya wiki iliyopita kuwa Kaseja yuko huru kurudi
Simba kwani ni sawa na nyumbani kwake.
0 comments:
Post a Comment