MSHAMBULIAJI wa Simba na mfungaji bora wa ligi kuu
soka Tanzania bara msimu uliopita, Mrundi Amissi Tambwe amekiri ugumu wa
kutetea kiatu chake cha dhahabu msimu huu.
Tambwe aliyetwaa ufungaji bora kwa kutia kimiani
mabao 19 alisema kufikia raundi ya tano msimu uliopita alikuwa tayari ameshatia
kamabani mabao yapatayo sita, lakini msimu huu anayeongoza kwa mabao (Didier
Fortune Kavumbagu-Azam fc) amefunga magoli manne tu.
“Ligi imekuwa ngumu sana, nakumbuka muda kama huu
msimu uliopita nilikuwa nimefunga mabao kama sita hivi, lakini angalia sahizi
anayeongoza ana mabao manne,”Alisema Tambwe.
“Lengo la ‘straika’ yeyote ni kufunga magoli, hata
mimi najitahidi kurudisha kasi yangu ya kufunga magoli, lakini ligi ni ngumu”.
Mrundi huyo aliongeza kuwa matokeo wanayopata
Simba ni ya kawaida katika mpira kwasababu hata timu kubwa kama Manchester
United hukumbwa na hali kama hii.
“Duniani kote, kuna wakati timu zinapitia wakati
mgumu, kwetu sisi ni changamoto. Tunajiandaa vizuri kwa mechi ijayo na lazima tushinde”.
Aliongeza Tambwe.
Simba inajiandaa kuchuana na Ruvu Shootings mwishoni
mwa wiki hii katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Mpaka sasa klabu hiyo ya Msimbazi, Kariakoo, Dar
es salaam imetoa sare katika mechi zote sita ilizocheza.
0 comments:
Post a Comment